Dunia inapita kipindi kigumu katika kuheshimu haki za binadamu: Kamishina Zeid

Dunia inapita kipindi kigumu katika kuheshimu haki za binadamu: Kamishina Zeid

Kuibuka kwa vikundi vyenye misimamo mikali kumeathiri namna serikali zinavyoshughulikia haki za binadamu amesema kamishna wa hakiza binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Hussein.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa Kamishna Zeid amesema serikali nyingi zinashinikiza asasi za kiraia kama sehemu ya kutowesha mitizamo ya misimamo mikali lakini badala yake huzalisha itikadi hizo.

Amesema  misuguano hiyo inaleta changamoto za kipekee na hivyo akashauri

(SAUTI ZEID)

‘‘Kuendelea kutoa usaidizi na kulinda haki za binadamu na hii inahitaji kazi ya mara kwa mara. Moja ya changmoto kubwa ni kwamba serikali haziko tayari kupokea changamoto kutoka vyanzo vingine mbali na Umoja wa Mataifa.’’