Skip to main content

Mashambulizi dhidi ya watetezi wa Amani Vietnam yatia mashaka:UM

Mashambulizi dhidi ya watetezi wa Amani Vietnam yatia mashaka:UM

Ofisi ha haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imesema inatiwa hofu na kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya watetezi wa Amani nchini Vietnam na jinsi uongozi wa nchi hiyo ulivyoshindwa kuchunguza na kuwachukulia hatua wahusika.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo shambulio la tatu tangu mwezi Septemba limetokea Jumapili iliyopita ambapo Bwana Nguyen Van Dai,mwanasheria maarifu na watetezi wengine watatu wa Amani walipokuwa wakiendesha mafunzo kwenye wilaya kwa watetezi wa haki za binadamu. Baada ya mafunzo kundi la watu 20 waliokuwa na magongo waliwashambulia wanaharakati wa kupigania amani wanne. Ravina Shamdasan msemaji wa ofisi ya haki za binadamu anafafanua Zaidi

(SAUTI YA RAVINA SHAMDASANI)

"Tunaitaka serikali ya Vietnam kuchukua hatua za dharura kuhakikisha usalama dhidi ya watetezi wa haki za binadamu na kuendesha uchunguzi wa kina na usioegemea upande wowote kuhusu matukio yote yalitoripotiwa yakihusisha watetezi wa haki za binadamu."