Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba kutoka Paris sasa ni kesho, mashauriano yanaendelea

Mkataba kutoka Paris sasa ni kesho, mashauriano yanaendelea

Mkataba mpya wa mabadiliko ya tabianchi sasa unatarajiwa kesho Jumamosi baada ya mashauriano ya usiku kucha kuamkia Ijumaa kuibuka na rasimu ambayo itajadiliwa na hatimaye kuweza kupitishwa Jumamosi.

Rais wa Mkutano huo Laurent Fabius wa Ufaransa amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari akikiri kuwa mashauriano ni magumu lakini ana matumaini kuwa yatazaa matunda.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye amekuwa akishiriki mashauriano ya kando na wajumbe wakiwemo mawaziri wa Mazingira, amekiri ugumu katika masuala kama vile uchangishaji fedha na nani wa kugharimika lakini..

(sauti ya Ban)

Nasihi wajumbe wa mazungumzo kuamua kwa kuzingatia dira ya dunia, huu si wasaa wa kuzungumzia mitazamo ya kitaifa. Suluhu bora za dunia zitaleta suluhu bora za kitaifa.”

Mmoja wa wajumbe ni Dokta Wilbur Ottichilo ni mwenyekiti wa mtandao kuhusu nishati endelevu na mabadiliko ya tabianchi kutoka Kenya.

(Sauti ya Dokta Ottichilo)