Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna changamoto nyingi Nigeria, lakini ni wakati wa matumaini- Ban

Kuna changamoto nyingi Nigeria, lakini ni wakati wa matumaini- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa ingawa kuna changamoto nyingi nchini Nigeria kama vile kuongezeka vitendo vya itikadi kali katili, kuna matumaini sasa.

Ban amesema hayo Jumapili akikutana na magavana wa majimbo ya Nigeria mjini Abuja.

Bwana Ban ambaye ameanza ziara yake nchini Nigeria hapo jana, amesema magavana wa Nigeria wana jukumu muhimu katika kuweka mustakhabali stahiki kwa nchi yao.

Katibu Mkuu amewapongeza viongozi wa Nigeria kwa kuhamisha mamlaka kutoka serikali moja hadi nyingine kwa njia ya Amani, kufuatia uchaguzi wa mwezi Aprili mwaka huu, akisema kuwa hatua hiyo ilitoa ishara ya matumaini kwa bara zima la Afrika.

Aidha, Bwana Ban amesifu makubaliano yaliyoafikiwa mwezi huu na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu malengo 17 ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.