Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio lapitishwa kuwajibisha wahusika wa ukatili Sudan Kusini

Azimio lapitishwa kuwajibisha wahusika wa ukatili Sudan Kusini

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linaloitaka ofisi ya haki za binadamu ya umoja huo kutume ujumbe wa kubaini na kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo.

Azimio hilo limepitishwa bila kupigiwa kura ambapo wajumbe wamesema wamezingatia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu pamoja na vitendo vya ukatili vilivyoripotiwa dhidi ya raia tangu kuanza kwa mzozo nchini humo mwezi Disemba mwaka 2013 na hivyo wanachotaka ni wahusika wawajibishwe.

Wajumbe wameitaka serikali ya Sudan Kusini kuipatia ushirikiano jopo la uchunguzi litakakwenda kufanya kazi hiyo na kutaka ofisi ya haki za binadamu kuripoti matokeo katika kikao kijacho cha 30 cha baraza hilo la haki za binadamu.

Balozi Keith Harper ni mwakilishi wa Marekani kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi na anafafanua kuhusu azimio hilo.

 (Sauti ya Balozi Harper)

"Tumeratibu pendekezo la ujumbe huu ili uwezeshe Baraza la haki za Binadamu kufuatilia na kuripoti hali ya kibinadamu na kuchukua hatua za kina kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa lengo la kuhakikisha uwajibikaji. Pia azimio linaweka vigezo vya ni vitu gani Baraza linapaswa kufuatilia."