Harakati za kukabiliana na Malaria Afrika Mashariki

24 Aprili 2015

Siku ya Malaria duniani tarehe 25 mwezi Aprili ni fursa kwa Shirika la afya duniani, WHO kuungana na wadau wengine wa afya ulimwenguni katika kutoa msukumo mpya wa kukomesha ugonjwa wa malaria. Kiasi cha watu  bilioni 3.2 kote duniani wako hatarini kuambukizwa malaria idadi ambayo ni sawa na nusu ya wakazi wa dunia. Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya malaria kwa mwaka huu ni wekeza katika mustakhbali, tokomeza Malaria ambapo WHO inasema  mwaka 2013 kulikuwa na visa milioni 198,  zaidi ya watu laki tano walifariki dunia.

Shirika hilo la  afya ulimwenguni linasema kuongezeka kwa kinga na juhudi za kudhibiti zimepunguza kwa asilimia 47 maambukizi kwa wanawake wajawazito tangu mwaka 2000 na kwa asilimai 54 barani  Afrika

Takwimu za WHO zinasema kuwa watu wanaoshi katika nchi maskini ndiyo wako hatarini zaidi ya kuambukizwa malaria ambapo mwaka 2013 asilimia 90 ya vifo vyote barani Afrika husuani kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano vilisababishwa na malaria.  Je hali ikoje Afrika Mashariki katika kupamabana na ugonjwa huu? Tuanzie Uganda ambapo John Kibego anasimulia juhudi za mapambano hayo .

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter