Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi mkuu Togo uwe wa amani, huru na wazi:

Uchaguzi mkuu Togo uwe wa amani, huru na wazi:

Katika mkesha wa uchaguzi mkuu wa Uraisi nchini Togo, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha kwamba uchaguzi huo unakuwa wa Amani, huru na wazi na unaozingatia matakwa ya watu wa Togo.Ban amewataka viongozi wote wa kisiasa na wafuasi wao kumaliza tofauti zao ambazo zinaweza kujitokeza katika mchakato wa uchaguzi kupitia katika na njia za Amani.

Pia amerejerea wito kwamba Umoja wa mataifa utaendelea kusaidia mchakato wa uchaguzi na juhudi za serikali ya Togo za kuimarisha demokrasia katika taifa hilo.