Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fahari ya kuwa msichana yabadili mtazamo wa afya ya uzazi Tanzania

Fahari ya kuwa msichana yabadili mtazamo wa afya ya uzazi Tanzania

Kuelekea siku ya wanawake duniani tarehe Nane mwezi huu, programu ya Fahari ya kuwa msichana inayotekelezwa nchini Tanzania imewezesha wasichana kubadili mtazamo wao kuhusu afya ya uzazi na hivyo kuwaepusha na mimba katika umri mdogo.

Catherine Fidelis ambaye ni Afisa kwenye mradi huo ulio chini ya taasisi ya Jane Goodall amesema mradi huo unaimarisha utoaji wa elimu ya afya ya uzazi kwani licha ya kutolewa shuleni bado inakumbwa na mkwamo kwa kuwa..

(Sauti Catherine-1)

Catherine amesema kuna mabadiliko kwani..

(Sauti Catherine-2)

Hadi sasa mradi huo kupitia Roots and Shoots unaogusia pia masuala ya uongozi, uchumi umefikia wasichana 300 wa kike katika mikoa ya Dar es salaam, Mara na Pwani.

Ujumbe wa siku ya wanawake duniani mwaka huu ni wezesha mwanamke, wezesha ubinadamu, pata picha!