Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSOM yalaani shambulizi dhidi ya hoteli Mogadishu

UNSOM yalaani shambulizi dhidi ya hoteli Mogadishu

Shambulizi dhidi ya hoteli kuu ya Mogadishu lililodaiwa na kundi la Al-Shabaab limewaua na kuwajeruhi makumi ya watu, wakiwemo viongozi wa serikali ya Somalia. Shambulizi hilo lilifanyika wakati wahanga hao wakijumuika kwa ajili ya sala ya ijumaa.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Nicholas Kay, amelaani vikali tukio hilo la kigaidi, akisema lililenga kuwakatisha tamaa Wasomali juu ya mustakhbali wao.

Aidha Kay amesema Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM utaendelea kuwasaidia Wasomali, wakati ambapo Somalia imeanza kufanikiwa katika kujenga upya mamlaka za serikali na nguvu zao za kijeshi, baada ya miaka zaidi ya ishirini ya vurugu.

Mkuu wa UNSOM amepeleka salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga, pamoja na serikali na raia wa Somalia.