UNMISS yalaani shambulio lililouwa watu 11 wakiwamo wanahabari

27 Januari 2015

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umelaani vikali mauaji ya raia kumi na mmoja, watano miongoni mwa wakiwa ni wanahabari ambao walishambuliwa barabarani wakati wakiwa wanasafiri kuelekea Raja jimboni Bahr El Ghazal MagharibiKwa mujibu wa taarifa ya UNMISS watu wasiofahamika na amboa walijihami kwa silaha walifyatua risasi katika msafara huo uliokuwa na magari mawili ambao ulikuwa ukimsafirisha kamshina mpya wa kata ya Raja, James Benjamin pamoja na waandishi hao.

UNMIS inasema hili ni shambulio la pili ndani ya wiki mbili na limefanyika kati aya eneo liitwalo Sepo na Magaya.

Ujumbe huo umetoa salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na kutoa wito kwa mamlaka za kitaifa na eneo husika kuchunguza tukio hilo ili kuwafikisha katika vombo vya sheria watekelezaji wa mauaji.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter