Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya haki za watoto kutathimini utekelezaji wa haki hizo

Kamati ya haki za watoto kutathimini utekelezaji wa haki hizo

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya haki za watoto inakutana Geneva kuanzia January 12 hadi 30 kutathimini hali ya haki za watoto katika baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania, Gambia na  Mauritius. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(TAARIFA YA GRACE)

Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo inayoundwa na wataalam huru 18, inatathimini namna nchi zimetekeleza mkataba wa watoto kulingana na majukumu ya mkataba wenyewe. Kamati pia inatathimini namna nchi zinavyotekeleza itifaki mbili za hiari mojawapo ikiwa ni uuzwaji wa watoto, picha za ngono kwa watoto,  utumikishwaji wa watoto katika ngono pamoja na utumikishwaji wa watoto katika vita.

Miongoni mwa nchi zinazotarajiwa kutathiminiwa ni Tanzania ambapo Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wa Tanzania, Pindi Chana amesema, japo serikali imetunga sera za kuwalinda watoto, bado kuna changamoto akitolea mfano wa masomo ya bure

(SAUTI PINDI CHANA)

Nchi wanachama wa mkataba  na itifaki za hiari  zinapaswa kuwasilisha taarifa ya maandishi  kwa kamati. Wakati wa mkutano mjini Geneva wajumbe wa kamati huwahoji maswali wawakilishi wa serikali husika.