Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Banbury ataka ushirikiano katika mapambano dhidi ya Ebola

Anthony Banbury, mkuu wa UNMEER. Picha ya UNMEER.

Banbury ataka ushirikiano katika mapambano dhidi ya Ebola

Mkuu wa ujumbe mpya wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia dharura ya ugonjwa wa Ebola (UNMEER) Anthony Banbury, amesema kazi ya kwanza ya UNMEER ni kushirikiana na mamlaka za serikali za Guinea, Liberia na Sierra Leone katika mapambano dhidi ya Ebola.

Akiongea baada ya kuwasili mjini Accra, Ghana tayari kuanza kuongoza ujumbe huo, Bwana Banbury, amewashukuru viongozi wa Ghana kwa kutambua umuhimu wa mlipuko wa Ebola na kukubali kusaidia Umoja wa Mataifa katika kuanzisha ujumbe huo mpya.

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya mawasiliano wa Ghana, Dkt Edward Boamah amekaribisha ujumbe wa Umoja wa Mataifa akisema ugonjwa wa Ebola ni shida ya kimataifa kwani hauna mipaka.

Mkuu wa ujumbe wa UNMEER anatarajiwa kuwasili Liberia Jumatano.

Idadi ya waliofariki dunia kutokana na Ebola imefikia 3,000