Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ebola: Ishara ya matumaini Nigeria na Guinea

Muuguzi akimfariji mgonjwa aliyethibitika kuwa na kirusi cha Ebola.(Picha: WHO/Chris Black)

Ebola: Ishara ya matumaini Nigeria na Guinea

Shirika la afya duniani, WHO limetoa taarifa likisema kuwa kwa sasa hakuna taarifa mpya ya maambukizi ya kirusi cha ugonjwa wa Ebola huko magharibi mwa Afrika kulikoripotiwa mkurupuko wa ugonjwa huo.

Ugonjwa huo uliibuka Guinea, Liberia, Sierra Leone na Nigeria ambako mjini Lagos hali ya Nafuu imeanza kupatikana kwani kupona kwa kwa mmoja wa walioambukizwa Ebola kumeondoa dhana potofu ya awali ya kuwa kuambukizwa ebola ni sawa na adhabu ya kifo.

Ushahidi wa awali unaonyesha kugunduliwa mapema sambamba na tiba ya mapema vinaweza kuongeza nafuu ya mtu kuishi japo ameambukizwa.

WHO inasema hali nchini Guinea ni nafuu kutokana na uelewa mkubwa wa umaa kuhusu ugonjwa huo ikilinganishwa na nchi Sierra Leone na Liberia.

 .