Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulizi la bomu Abuja, Nigeria

UN Photo.
Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@

Ban alaani shambulizi la bomu Abuja, Nigeria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezea kushtushwa na shambulizi la bomu la Jumatano katika kituo cha biashara kwenye mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ambalo liliripotiwa kuwaua watu 21.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wake imesema kuwa Ban ametuma risala za rambi rambi kwa jamaa za wahanga na kuwatakia nafuu haraka walijeruhiwa.

Katibu Mkuu amerejelea kulaani vikali mashambulizi kama hayo, akiongeza kuwa anaendelea kutiwa wasiwasi na kuongezeka kwa ukatili kama huo nchini Nigeria.