Ban awapongeza Walibya kwa uchaguzi na kulaani ghasia

Picha: UNSMIL/Lason Athanasiadis(UN News Centre)

Ban awapongeza Walibya kwa uchaguzi na kulaani ghasia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametuma risala za pongezi kwa watu wa Libya kwa uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amesema uchaguzi huo ni hatua muhimu katika kupeleka harakati za mpito mbele, na kuweka utulivu katika harakati za kisiasa

Bwana Ban amewasifu wadau wote kwa kutoa fursa ya kuwezesha uchaguzi huo muhimu.

Hata hivyo, Bwana Ban amemulika suala la machafuko yanayoendelea nchini Lybia, yakiwemo matukio kadhaa kwenye siku ya uchaguzi, na kulaani vikali mauaji ya Bi Salwa Bugaighis, ambaye amemtaja kama mtetezi jasiri na anayeheshimika wa haki za binadamu, ambaye alichangia pakubwa katika maandamano ya mapinduzi ya Februari mwaka 2011 nchini Libya.