Umoja wa Mataifa walaani shambulio la kujilipua Lebanon

24 Juni 2014

Derek Plumbly ambaye ni Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon amelaani vikali kisa cha shambulio la kujilipua kilichotokea jana kwenye viunga vya mji mkuu Lebanon na kusabisha kifo cha mlinzi mmoja na majeruhi kadhaa.

Ofisi ya Plumbly imesema shambulio lilitokea karibu na kituo cha ukaguzi cha jeshi la Lebanon kwenye mzunguko wa Tayaouneh kusini mwa Beirut.

Bwana Plumbly amesisitiza umuhimu wa umoja nchini Lebanon hasa wakati huu wa  vitisho vya kigaidi.

Halikadhalika, amewapongeza wanajeshi wa nchi hiyo kwa kujitolea kwao, kwa kulinda na kudumisha utulivu na usalama na akasisitiza tena kwamba Umoja wa Mataifa utaendeleza mshikamano na serikali ya Lebanon na wananchi wake wanapojizatiti kukabiliana na vitisho vya ugaidi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter