Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lithuania ilikiuka haki za kisiasa-UM

Lithuania ilikiuka haki za kisiasa-UM

Lithuania imetajwa kuvunja kwa haki za msingi za kisiasa pale ilipopitisha sheria iliyompiga marafuku kwa mtu yoyote aliyeondolewa kwenye utumishi wa umma kutowania nafasi yoyote ya uongozi, sheria ambayo ilipitishwa mara tu baada ya kuondolewa madarakani kwa nguvu kwa raia wa wakati huo Rolandas Paksas .

Kulingana na kamati ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu taifa hilo lilikwenda kinyume na sheria za kimataifa kwa kupitisha sheria ambayo iliwanyima fursa baadhi ya raia wake kuwania madaraka ya juu.

Kamati hiyo ilifikia uamuzi huo kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwenye kamati hiyo na Paksas ambaye aliondolewa madarakani kwa amri ya bunge Aprili 2004.

Mwanasiasa huyo Paksas alitaka kubatilishwa kwa sheria hiyo akisema kuwa ilianzishwa kwa nia mbaya na ambayo ilimlenga yeye binafsi.