Mtaalam wa masuala ya ukatili dhidi ya wanawake kuzuru Uingereza

28 Machi 2014

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za wanawake, Rashida Manjoo, atatembelea Uingereza kati ya March tarehe 31 na April 15, kwa ajili ya kuangalia hali ya ukatili wa kifamilia na wa kingono, kama mfano ukeketaji wa wanawake na wasichana , pamoja na ndoa za utotoni.

Ukatili dhidi ya wanawake ni moja wapo wa ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu, na hutokea popote duniani, amesema Bi Manjoo, akiwa ni mtaalam wa kwanza kufanya ziara kutoka baraza la haki za binadamu nchini Uingereza.

Mtaalam huyo ameeleza kwamba atakutana na watu na mashirika yanayohusika katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake, nia yake ikiwa ni kupima ukubwa wa utekelezaji wa tabia hizi ndani ya nchi ya Uingereza.

Bi Manjoo, ambaye ni raia wa Afrika ya Kusini, atachungulia pia ukatili unaotekelezwa na serikali, pamoja na kuangalia changamoto mpya zinazotokea na uingiliaji nchini wa wanawake wahamiliaji na wakimbizi.

Mtaalam huyo amealikwa na serikali ya Uingereza. Atatembelea maeneo ya London, Edinburgh, Glasgow, Belfast, Cardiff and Bristol, na kisha atatoa repoti yake mbele ya baraza la haki za binadamu.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter