Hali katika CAR yamulikwa kwenye Baraza la Usalama

6 Machi 2014

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kwa ajili ya hali katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku wanachama wake wakisikiliza ripoti za hali halisi nchini humo. Joshua Mmali na taarifa kamili

TAARIFA YA JOSHUA

Ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu hali katika CAR, imewasilishwa na Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa, Herves Ladsous, ambaye amesema changamoto za CAR ni nyingi

“Hakuna jeshi la kitaifa, na askari polis walosalia hawa vifaa vya kutekeleza majukumu yao. Vikosi vya uslama vya kimataifa vilivyopelekwa huko kwa sasa havitoshi. Havina kitengo cha wahudumu wa kiaraia ili kukabiliana kikamilifu na ulinzi wa raia na pia vianzo vya mzozo uliopo”

Ripoti ya Katibu Mkuu inapendekeza kuubadili ujumbe uliopo sasa nchini humo MISCA ili uwe ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wenye wanajeshi elfu kumi na askari polisi 1,820, hatua ambayo inakadiriwa kuchukua takriban miezi sita. Ripoti hiyo Irasema hali katika CAR imebadilika katika miéis michache ilotita, na hali ya usalama kuzorota zaidi, kwani raia wanaendelea kuuawa kila siku, na wengine kulazimika kuhama makwao.

Mkutano wa Baraza la Usalama pia umehutubiwa na Mkuu wa Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA, Valerie Amos na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, Antonio Guterres.