Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rasilimali watu yahitajika zaidi kukagua silaha za nyukilia Iran : IAEA

Rasilimali watu yahitajika zaidi kukagua silaha za nyukilia Iran : IAEA

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA Yukiya Amano amesema wanahitaji kuongeza rasilimali watu ili waendane na ongezeko la kazi ya ukaguzi wa silaha za nyukilia nchini Iran.

Bwana Amano ameiambia bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo  mjini Vienna, Austria kuwa  wakaguzi watahitaji kuyafikia maeneno zaidi na kwamba watahitaji kufunga vifaa zaidi vya ulinzi na kuchambua sampuli huku pia akisema kazi yauchambuzi na kutoa taarifa itaongezeka.

(SAUTI YUKIYA AMANO)

Tunatarajia kutumia takribani euro nusu milioni ya garama za zaidi katika idara ya vifaa vya ulinzi katika kutoa kipaumbele kwa kazi yetu, kupanga upya kazi na kuahamisha wafanyakazi lakini shirika litahitaji bajeti ya ziada ya euro milioni 5.5 kwa ajili ya kipindi cha miezi sita

Mnamo tarehe 24 Novemba mwaka jana,China, Ufaransa, Ujerumani, Urusi, Uingereza na Marekani zilikubaliana naIran  katika mpango wa ufumbuzi wa silaha za nyuklia nchini humo, mpango unaoratibiwa na IAEA.