Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Virusi vya kidingapopo aina ya 3 vyaibuka tena kusini mwa Pacific

Virusi vya kidingapopo aina ya 3 vyaibuka tena kusini mwa Pacific

Virusi vya homa ya kidingapopo aina ya 3 vimeibuka tena katika nchi kadhaa za Kusini mwa Pacific baada ya karibu miongo miwili. Idadi ya visa inatarajiwa kuendelea katika miezi ijayo kwenye maeneo mengi ikiwemo kuongezeka Fiji, French Polynesia na Kiribati, wakati mlipuko mkubwa kwenye visiwa vya Solomon unamalizika.

Hivi sasa wizara za afya za mataifa ambayo yameathirika yanajitahidi kuelimisha jamii jinsi ya kuzuia homa ya kidingapopo na kuwapa mafunzo ya kuwakumbusha wahudumu wa afya , kubaini na jinsi ya kutibu dalili za homa hiyo.

Kuna aina nne za virusi vinavyosababisha homa ya kidingapopo, kuambukizwa na aina moja kutatoa kinga ya maisha dhidi ya aina hiyo, lakini sio kwa aina zingine tatu.

Aidha watoto wanaozaliwa ambao hawajaambukizwa na aina Fulani ya homa ya kidingapopo , wanaunda kundi Fulani. Hivyo sio kitu kipya kwa aina za homa ya kidingapopo kuibuka tena huko Pacific baada ya kutokomezwa kwa takribani miaka 15 au 20, inawezekana ni kwa sababu idadi ya wasioambukizwa inadizi ya wale waliowahi kupata homa hiyo.

Homa ya kidingapopo inaambukizwa kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes ambaye mara nyingi huuma mchana na haiambukizi kutoka binadamu mmoja kwenda mwingine. Dalili zake ni mafua, homa kali, kuumwa kichwa, kuumwa macho, kichefuchefu na kutapika, maumivu ya mifupa au misuli na kupata vipele.