Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washutumu makundi ya wanamgambo Syria kutekeleza mauaji ya halaiki

UM washutumu makundi ya wanamgambo Syria kutekeleza mauaji ya halaiki

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa inashutumu makundi ya wanamgambo yanayoendesha shughuli zao ndani ya Syria kutekeleza mauaji ya umati wa raia na wafungwa inaowashikilia. Flora Nducha na habari kamili

 (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Ofisi ya haki za binadamu inasema imepokea taarifa za mfululizo wa mauaji ya umati wa raia na wapiganaji ambao hawashiriki tena katika mapigano mjini Idlib na Raqqa. Mauaji hayo yamearifiwa kufanywa na makundi ya upinzani yenye itikadi kali hususani kwenye mataifa ya Kiislam yaIraqnaSyria(ISIS).

Kamisha wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameonya makundi hayo yanayotekeleza mauaji, kwamba yanakiuka sheria za kimataifa za hakim za binadamu na hatua zao zinaweza kuwa uhalifu wa vita. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu mjiniGeneva.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

“Inaonekana kuna desturi inayoibuka ambapo, wakati makundi hayo yamekuwa katika vitisho toka kwa makundi mengine , au yamefukuzwa kutoka katika eneo fulani, yamekuwa yakitekeleza mauaji ya baadhi au wafungwa wote walionao katika maeneo yao, na hii imedhihirika kutokea kwa Aleppo .Walikuwa wanatumia hospitali ya watoto kama makao yao na walipolazimishwa kuondoka wakati makundi mengine ya upinzani yaliposhambuliwa, inaonekana walikuwa wameshauwa idadi kubwa ya watu katika eneo hilo. Hawa ni wafungwa, ni watu waliowakamata, ambao wamekuwa wanawashikilia na kuwauwa . Kwa hakika ni kinyume na sheria za kimataifa au pengine ni uhalifu wa vita.Tunajaribu kuwaeleza bayana kwamba waoko kama mtu mwingine yeyote na wanawajibika kuheshimu sheria za kimataifa. Na kama kuna uhalifu wa vita , ushahidi utakusanywa na watakabiliwa na mashitaka kwa kosa hilo.”

Kamishina mkuu amerejea kutoa wito kwa pande zote nchiniSyriakuwatendea vyema watu inaowashikilia , kwa utu na kuwaachilia mara moja wale wote wanaonyimwa uhuru wao kwa kukikuka sheria za kimataifa.