Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini inaweza kutumbukia kwenye tatizo la njaa-FAO

Sudan Kusini inaweza kutumbukia kwenye tatizo la njaa-FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limeonya kuwa hali ya mapigano inayoendelea sasa huko Sudan Kusini inaweza inaweza kusababisha kuzuka kitisho cha njaa .

FAO inasema kuwa hali ya misaada ya kibinadamu nchini humo kwa wakati huu imeendelea kuzorota na kwamba kunauwezekano mamia ya raia wakaendelea kupoteza maisha kutokana na kukosa mahitaji muhimu.

Mapigano hayo yamefanya shughuli za usambazaji wa misaada kusimama katika baadhi ya maeneo na ripoti zinasema kuwa hali kwa ujumla ni mbaya.

Mwakilishi wa FAO nchini Sudan Kusin Sue Lautze amesema kuwa kuna matatizo mengi yanayoendelea kuikabili nchi hiyo ikiwemo baadhi ya mifugo kukubwa na magonjwa.