Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wa Syria ulishudiwa kwa mwaka wa tatu mfululizo

Mzozo wa Syria ulishudiwa kwa mwaka wa tatu mfululizo

Nchini Syria, mzozo ulioanza takriban miaka mitatu ilopita ulifikia upeo mpya mwaka huu wa 2013.

La kutisha zaidi katika mzozo huo ni kwamba, ni katika mwaka huu ndipo kwa mara ya kwanza, kuliripotiwa matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria, ambapo watu wengi waliathirika katika tukiohilo. Tukio hilo lilimfanya Katibu Mkuu kuunda tume ya uchunguzi katika matumizi ya silaha hizo, ikiongozwa na Profesa Ake Sellstrom, ingawa serikali yaSyriahaikutoa ushirikiano wa haraka. Bwana Ban akasema…

 (Sauti ya Ban)

Huku idadi ya watu wanaolazimika kuhama makwao ikiwa watu elfu tano kila siku, kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, idadi ya wakimbizi wa Syria ilipanda kwa takriban milioni moja nukta nane katika kipindi cha miezi kumi na miwili na kuzidi milioni mbili mnamo mwezi Septemba mwaka huu. Wakati huo, Kamishna Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres alisema kuwa mzozo wa Syria umekuwa janga la kibinadamu la kutia aibu, na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa izisaidie nchi zinazowapokea wakimbizi wa Syria.

 (Sauti ya Guterres)

Mahitaji ya kibinadamu nayo yalizidi kupanda, huku jinsi ya kuwafikia wanaohitaji misaada hiyo ikiendelea kuwa ngumu, kwa mujibu wa Ofisi ya Kuiratibu Masuala ya Kibinadamu, OCHA.