Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi Sudani Kusini washerehekea krisimasi kambini

Wakimbizi Sudani Kusini washerehekea krisimasi kambini

Tarehe 25 na 26 mwezi huu wakristo duniani waliungana katika kuadhimisha sikukuu ya Krismasi yaani kuzaliwa kwa Yesu Kristo, ambaye kwa mujibu wa msingi wa imani yao ndiye mwokozi wa ulimwengu. Sikukuu hii ambayo hutumiwa na watu wengi duniani kujumuika pamoja na ndugu, jamaa na marafiki iliwakuta maelfu ya raia nchini Sudani Kusini wakiwa wakimbizi kufuatia mapigano nchini humo.

Licha ya kuwa katika kambi ya wakimbizi, raia hawa waliadhimisha sikukuu hii huku wakipewa ujumbe wa kupendana na kusameheana. Ungana na Joseph Msami katika ripoti inayoangazia krismasi katika kambi ya wakimbizi.