Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama kukutana leo kujadili kuimarisha UNMISS

Baraza la usalama kukutana leo kujadili kuimarisha UNMISS

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Hilde Johnson, leo amekuwa na mkutano na waandishi wa habari mjini Juba kuelezea hali halisi hivi sasa wakati ambapo raia Elfu 81 wamepoteza makazi yao tangu kuanza kwa mzozo huo zaidi ya wiki moja. Hayo yamefanyika wakati Baraza la Usalama likitarajiwa kukutana baadaye Jumanne kujadili ombi la Katibu Mkuu la kuimarisha uwezo wa kijeshi wa kikosi cha UNMISS ili kulinda raia.