China yapiga hatua kuwaendeleza wanawake, lakini bado inakabiliwa na changamoto

24 Disemba 2013

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika utokomezaji wa mifumo yote inayowakandamiza na kuwabagua wanawake limesifu namna Chinailivyopiga hatua kuendeleza ustawi wa wanawake, lakini hata hivyo limesema kuwa  bado kuna mengi yanapaswa kufanywa. Grace Kaneiya na taarifa kamili

 (TAARIFA YA GRACE)

Limesema kuna hali ya kusua sua juu ya utekelezaji kwa vitendo baadhi ya sheria na katika maeneo mengine hakuna mikakati ya dhati kuwaendeleza wanawake ili washiriki kwa uhuru katika majukuwaa ya kisiasa na kumiliki vyanzo vya kiuchumi.

Katika taarifa yake jopohilolimesema kuwa wakatiChinaikipiga hatua kusonga mbele kimaendeleo, kuna kundi kubwa la wanawake limesalia nyuma likiandamwa na changamoto zilizosababishwa na ukosefu wa fursa sawa kwa wote.

Taarifa hiyo ya wataalamu imekuja mwishoni mwa ziarayaoya siku nane iliyodumu kuanzia Disemba 12 hadi 19.Ikiwa ni ziarayaoya kwanza nchini humo wataalamu hao walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali na kufanya tathmini.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter