Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yatilia shaka juu ya kuongezeka vitisho kwa raia Saudia Arabia

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yatilia shaka juu ya kuongezeka vitisho kwa raia Saudia Arabia

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa imeingiwa na wasiwasi kuhusiana na ripoti ya kuongezeka kwa vitendo vya vitisho kwa makundi ya raia nchini Saudia Arabia.

Pamoja na kuandamwa na vitisho raia hao pia wamekuwa wakikabiliwa na njama ya kuteswa na kutupwa gerezani. Serikali ya Saudia Arabia inalaumiwa kuwa kuendelea kubana uhuru wa maoni kwa wananchi wake.

Pia kuna taarifa za kufanyika kwa kesi katika mazingira ya siri na washtakiwa kutupwa gerezani bila kupewa fursa za kujitetea na kuwakilishwa na wanasheria wao.

Kutokana na hali hiyo, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa inaingia hofu na taarifa za kuongezeka kwa vitendo hivyo.