Pillay agadhabishwa kutokana na kuharamishwa kwa uhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja

12 Disemba 2013

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameghadhabishwa na hatua ya india ya kutangaza kuwa uhalifu uhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja kotokana na uamuzi wa mahakama kuu . Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Pillay amesema kuharamiswa kwa  uhusino wa kimapenzi wa jinsia moja ni ukiukaji wa haki zikiwemo za kijamii na kisisaa ambazo India ni mwanachama akiongeza kuwa hatua hiyo ya mahakama ni kama kupiga hatua nyuma na pigo kubwa kwa haki za binadamu.

Mahakama kuu nchini India ilikuwa imeombwa kutathmini kipengee cha 377 cha kanuni ya makosa ya jinai ambacho kinaruhusu kuadhibiwa kwa  wale wa jinsia moja wanaohusika kwenye uhusiano wa kingono.

Kwenye uamuzi wake mahakama kuu ilitangaza kipengee hicho cha 377 kuwa kisicho halali kwenye kanuni ya makosa ya jinai na kubatilisha  uamuzi wa Mahakama kuu wa mwaka 2009 hatua ambayo inaharamisha mapenzi ya jinsia moja.