Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atiwa wasiwasi na hali ya watawa wa kanisa la Ki-Orthodox Syria

Ban atiwa wasiwasi na hali ya watawa wa kanisa la Ki-Orthodox Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameelezea kusikitishwa na hali ya kushambulia maeneo ya ibada na wawakilishi wa kidini katika mzozo unaoendelea nchini Syria. Hali hiyo imedhihirishwa na hali ya watawa 12 ambao walitoweka kutoka makazi yao ya kanisa la Ki-Orthodox la Mtakatifu Tecla, Ma’aloula.

Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban ameongeza sauti yake kwa wito wa kuhakikisha usalama wa watawa hao na maslahi yao, na watu wengine wote ambao huenda wamezuiliwa bila hiari yao nchini Syria.

Amesema Umoja wa Mataifa unakataa hali yoyote ya kuwalenga watu kwa misingi ya dini, jamii au kabila lao, na kuongeza kuwa raia kote nchini Syria wamo hatarini na ni lazima walindwe.