Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres ataka maisha ya baadaye ya watoto wa Syria kutiliwa maanani

Guterres ataka maisha ya baadaye ya watoto wa Syria kutiliwa maanani

Kamishina mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, Antonio Guterres amelipongeza taifa la Lebanon kutokana na utu wake lilipojitolea kuwapa hifadhi zaidi ya watu 800,000 ambapo pia ameyataka mataifa wahisani kutoa misaada ya kifedha .

Mkuu huyo wa UNHCR ambaye tayari ameutembelea mji wa Arsal nchini Lebanon mji ulio bonde la Bekaa yaliyo makao kwa maelfu ya wakimbizi kutoka nchini Syria ameiomba jamii ya kimataifa kuwakaribisha wakimbizi kutoka Syria walio na nia ya kuingia kwenye nchi zao.

Ziara ya Guterres nchini Lebanon inajiri baada ya  ripoti iliyotolewa na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

Ripoti hiyo inaeleza jinsi watoto  walivyoathiriwa na vita kutokana na yale ambayo wameyashuhudia vitani huku asilima ndogo ya watoto wakiwa ndio wanasoma. Kwa sasa watoto milioni 1.1 nchini Syria ni wakimbizi.

Guterres ametaka hali ya baadaye ya watoto wa Syria kutiliwa maanani kuambata na ripoti na ripoti ya wiki iliyopita.