Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi waendelea na kuhama wakitafuta misaada nchini Ufilipino

Watu zaidi waendelea na kuhama wakitafuta misaada nchini Ufilipino

Maelfu ya  watu walionusurika kimbunga Haiyan kutoka maeneo ya Tacloban nchini Ufilipino wameripotiwa kuhama makwao wakitafuta wenzao na misaada kwenye maeneo yaliyo karibu na pia ya mabli kama Cebu naManilakwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

UNHCR inasema kuwa muda mfupi baada ya kimbunga kuikumba Ufilipino watu walianza kuondoka kwa njia ya bahari na ndege. Nazo ndege za mizigo zinazosafirisha misada kutokaCebukwenda Tacloban, Guiuan na maeneo mengine zimekuwa zikirudi na watu wengi kila siku. Adrian Edward kutoka UNHCR anaeleza.

 (SAUTI YA ADRIAN EDWARD