Muungano wa Afrika wapongeza azimio la Baraza la Usalama la UM

13 Novemba 2013

Mwakilishi maalum wa Muungano wa Afrika nchini Somalia, Balozi Mahamat Saleh Annadif ameunga mkono azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa MAtaifa la kuongeza muda wa vikosi vya muungano huo nchini Somalia, AMISOM hadi Oktoba mwaka 2014, pamoja na kuongeza usaidizi kwa jeshi la nchi hiyo. Alice Kariuki na taarifa kamili

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Balozi Annadif anasema kuwa uamuzi wa baraza hilo uajiri wakati wakati AMISOM na wanajeshi wa Somalia wamepiga hatua kubwa ya kuwatimua wanamgambo wa Al-Shabaab kutoka miji kadhaa nchini humo na kuelekea miji zaidi iliyo chini ya wangambo hao. Azimio hilo linakuja kufuatia ombi lililotolewa na baraza la amani na usalama la Muungano wa Afrika kupitia barua yake ya mwezi Oktoba mwaka huu ambapo liliomba kuongezwa kwa wanajeshi watakaowasaidia wanajeshi wa Somalia kuendelea na opereshi ya kuleta udhabiti nchini humo. Balozi Annadif ameongeza kuwa azimio hilo ni ishara kuhusu ni jinsi gani ulimwengu unavyochukulia kwa umuhimu jitihada za Muungano wa Afrika nchini Somalia na pia kama mwitikio kuwa AMISOM ina wajibu mkubwa kwenye vita dhidi ya ugaidi na uharamia. Amezishukuru nchi zinazotoa mchango wao na kuzitaka kushirikiana na kuongezeka wanajeshi zaidi.