Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ya hewa ya Ukaa yadorora, kupatiwa msukumo mpya

Biashara ya hewa ya Ukaa yadorora, kupatiwa msukumo mpya

Kikao cha kumi na tisa cha mkutano wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi kinaendelea mjini Warsaw, Poland, jitihada ikiwa ni kuibuka na makubaliano mapya yatakayokuwa jumuishi kuliko ya awali kama Kyoto ambayo hayajaweza kudhibiti uchafuzi wa mazingira duniani. Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya Kisayansi na Taaluma ya mkataba huo Dk. Richard Muyungi ameiambia Idhaa hii kutoka Warsaw kuwa ushiriki na uwazi katika makubaliano mapya ni muhimu na kuna matumaini.

(Sauti ya Dkt. Muyungi)

Dkt. Muyungi akazungumzia usiri wa biashara ya hewa ya Ukaa iliyobuniwa kupunguza gesijoto.

(Sauti ya Dkt. Muyungi)

Makubaliano mapya yanatakiwa yawe yamefikiwa ifikapo mwaka 2015 wakati wa kikao kitakachofanyika mjini Paris, Ufaransa.