Malefu ya raia wa DRC waingia Uganda wakikimbia oparesheni dhidi ya kundi la M23

5 Novemba 2013

Zaidi  ya watu 10,000 wamekimbia maeneo yaliyo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DCR kwenda nchini Uganda kufuatia mapigano  kati ya wanajeshi wa serikali na wanachama wa kundi la M23 kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.

 (TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Wanaohama makwao wanaingia kwenye wilaya ya Kisoro iliyo Kusini Magharibi mwa Uganda.

Wafanyikazi wa UNHCR walio mpakani wanasema kuwa mabomu yanaanguka karibu na mpaka na kuzua hofu miongoni mwa wale wanaokimbia na raia wa Uganda wanaoishi karibu na mpaka.

Zaidi ya nusu ya wakimbizi wa ndani ambao wamewasili kwenye kituoa cha Nyakabande ni watoto ambao wametenganishwa na familia zao wakikimbilia maeneo ya mpaka.

Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR mijini Geneva

Wakimbizi wengi wanasafiri kwa miguu kwenda kwa kituo. Kuna baridi na mvua na hali si nzuri. Kwa sasa kuna misaada ya dharura kwa watu 10,000. Zaidi na  mamia ya mahema kuna  makao ya muda yanayowahifadhi watu 300. Nyingine inajengwa. Wengi wa wanaowasili ni watoto na wengi wametenganishwa na familia zao wanapokimbia kutoka kwa mpaka. Hadi sasa tumepokea zaidi ya watoto 100 wakiwa peke yao na tumewahifadhi kwenye mahema tofauti na kuwasaidia kupata chakula na kuwaunganisha na familia zao.”