Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaokoa maisha ya mtoto Albino aliyekimbia DR Congo

UNHCR yaokoa maisha ya mtoto Albino aliyekimbia DR Congo

Kijana mmoja mwenye ulemavu wa ngozi au albino amelazimika kukimbia kutoka DR Congo si kutokana na machafuko bali kutokana na watu wanaodaiwa kumsaka ili wachukue viungo vyake kwa ajili ya ushirikina. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Anaclet ambaye ni baba mzazi wa kijana huyo aitwaye Jeff ameliambia shirika la kuhudumai wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR nchiniBurundikuwa wamekimbilia kituo  cha  muda cha wakimbizi cha Kajaga, hukoBujumburaili kuokoa maisha ya mwanae mwenye umri wa miaka Sita.

Tayari UNHCR inawapatia hifadhi na ulinzi ili kuondokana na kitendo cha kuhamahama ambapo Mwakilishi wa shirika hilo nchini Burundi, Catherine Huck amesema wakati umefika kwa serikali kuchukua hatua muafaka dhidi ya fikra potofu dhidi ya Albino na kuhakikisha wanalindwa ili haki zao za msingi kama vile elimu ziweze kuzingatiwa.