Baraza Kuu lasikiliza ripoti za mahakama za kimataifa za Rwanda na Yugoslavia

14 Oktoba 2013

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeombwa kushirikiana na mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, ICTR ili kuwapokea washukiwa waloachiliwa na wale ambao hawakupatikana na hatia, kama sehemu ya kuwahamisha kwa ajili ya usalama wao. Joshua Mmali ana maelezo zaidi

TAARIFA YA JOSHUA

Ombi hilo la mahakama ya ICTR, limewasilishwa na rais wa Mahakama hiyo, Jaji Vagn Joensen kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambalo limekutana leo kusikiliza ripoti za Katibu Mkuu kuhusu mahakama ya ICTR na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kuhusu Yugoslavia. Katika ripoti ya kumi na nane ya kila mwaka tangu kuzinduliwa mahakama ya ICTR, Jaji Joensen amesema kuwasaka na kuwafikisha mahakamani washukiwa watatu wakuu ambao ni Felicien Kabuga, Protais Mpiranya, na Augustin Bizimana imeendelea kuwa sehemu muhimu ya kazi ya kuendesha mashtaka katika mahakama hiyo. Hata hivyo, Jaji huyo amesema suala la kuwahamisha washukiwa waloachiliwa na wale ambao wamekamilisha kifungo chao nchini Tanzania bado ni la utata, kwani mahakama hiyo haijapata ushirikiano mzuri kutoka kwa jamii ya kimataifa.

“Suala hili limeendelea kuwa changamoto sugu, kwani hadi sasa hakujakuwa na hatua zozote za ufanisi. Msajili wa mahakama nami bado tuna utashi wa kufanya kila liwezekanalo ili kupata suluhu kwa tatizo hili, na tuna hofu kubwa kuhusu hatma ya kufeli kufanya hivyo. Narudia tena wito wa dharura wa ushirikiano zaidi kutoka kwa nchi wanachama katika juhudi za mahakama za kuwahamishia watu hawa nchi nyingine.”

Jaji Joensen amesema ana matumaini makubwa kuwa ni ripoti mbili tu nyingine zitaka