Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yasononeshwa na vifo vya wafanyakazi wa kiwanda Bangladesh

ILO yasononeshwa na vifo vya wafanyakazi wa kiwanda Bangladesh

Shirika la kazi duniani, ILO limeelezea kusikitishwa kwake na kufuatia vifo vilivyosababishwa na moto katika kiwanda cha nguo huko Aswad nchini Bangladesh.

Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mkuu ILO Guy Ryder amesema moto huo ulioathiri sekta ya nguo ambazo zimeshashonwa nchini Bangladesh umedhihirisha huzuni na ukweli kwamba juhudi zaidi zinahitajika kwa ajili ya usalama na afya ya wafanyakazi wa viwanda vya nguo.

Bwana Ryder amesisitiza kwamba licha ya vifo vya watu kwa miaka mingi iliyopita, bado wafanyakazi wanakufa na vifo hivyo vingeweza kuepukika ikiwa mazingira mazuri ya kufanya kazi yangeboreshwa.