Wajumbe wa Baraza la Usalama wapitisha mswada wa Syria:

28 Septemba 2013

Wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama na wale wasio wa kudumu Ijumaa jioni wamepiga kura ya mswaada wa azimio kuhusu silaha za kemikali nchini Syria.

(SAUTI YA RAIS WA BARAZA)

 Akizungumzia azimio hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kwa mujibu wa uchunguzi wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi wa matumizi ya silaha za kemikali , silaha hizo zimetumika Syria na kwa mantiki hiyo lazima hatua zichukuliwe

(CLIP BAN KI-MOON)

Kama tume iliyotumwa kwenda kuchunguza madai imethibitisha silaha za kemikali zilitumika Syria.Waliohusika lazima wafikishwe kwenye mkono wa sheria na jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa kuhakikisha kwamba silaha hizi za maangamizi hazitoibuka tena kama chombo cha vita au ugaidi.

Amesema azimio la leo litahakikisha zilaha hizo zinaangamizwa na mafanikio yake yatatokana na Syria kutoa ushirikiano unaohitajika

(CLIP BAN)

“ Serikali ya Syria lazima itimize wajibu wake, pande zote lazima zihakikishe ulinzi na usalama wa wakaguzi.Tukifikia hatua hii muhimu ni lazima tusisahau kwamba madhila Syria yanaendelea huku mabomu na vifaru, magruneti na bunduki. Kuzimwa kwa mfumo mmoja wa silaha hakumaanini ni ruksa kwa mingine.Hiki sio kibali cha kuua kwa silaha zingine. Machafuko lazima yakome na mitutu yote ya bunduiki lazima izimike”

Akizungumzia azimio hilo waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kery amesema azimio la leo linaonyesha kwamba panapo mshikamano uovu wowote utashindwa

(SAUTI YA JOHN KERRY)

Naye waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov akisisitiza umuhimu wa azimio la leo amesema

(CLIP LAVROV)

Kwa ujumla wajumbe wote wakiwemo pia waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague , Ufaransa, Uchina na wengineo wamesema hatua ya leo ya kupitisha azimio dhidi ya Syria ni ya kihistoria na silaha za kemikali hazina nafasi katika dunia hii. Wameunga mkono wito kwamba mateso na matatizo ya kibinadamu yanayowakabili mamilioni ya Wasyria ni lazima yakomeshwe mara moja.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter