Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban na waziri wa mambo ya nje wa Urusi wajadili suluhu ya mgogoro wa Syria

Ban na waziri wa mambo ya nje wa Urusi wajadili suluhu ya mgogoro wa Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon jioni ya leo Ijumaa amekutana na waziri wa mambo ya nje wa shirikisho la Urusi Sergey V. Lavrov.

Viongozi hao wawili wamejadili masuala mbalimbali Katibu Mkuu Ban amesisitiza haja ya kutafuta suluhu ya kisiasa katika mgogoro ambao sasa umekuwa wa muda mrefu wa Syria.

Pia amesema ni muhimu kumaliza madhila ayanayoendelea kuwakabili mamilioni ya watu wa taifa hilo wanaoendelea kushuhudia machafuko.

Kwa pamoja pia wamejadili athari za mgogoro huo wa Syria kwa mataifa jirani ikiwemo Lebanon ambayo imebeba mzigo mkubwa wa wakimbizi kutoka Syria.