Uganda yapata chuo cha uhamiaji ili kupanbana na uhalifu wa kimataifa

27 Septemba 2013

Katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kimataifa ukiwemo ugaidi na usafirishaji haramu wa binadamu, Uganda imeanzisha chuo cha uhamiaji ili kuimarisha usalama kwenye mipaka yake. John Kibego wa radio washirika ya Spice FM Uganda, ana ripoti kamili

(Tarifa ya John Kibego)

Chuo hiki kimezinduliwa kwenye eneo la chuo cha zamani cha jeshi la wanhewa na slaha za masafa marefu katika bonde la hufa la Ziwa Albera, kwenye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo (DRC). Akiongea kwenye sherehe ya uzinduzi, waziri wa mabo ya ndani Jenerali Aronda Nyakairima alisema, vitisho vya kigaidi, ulanguzi wa binaadamu na madawa ya kulevya ni changamoto sugu zinazoikabili nchi.

Jenerali Aronda alionyesha matumaini kuwa kupata mafisa zaidi wa Uhamiaji na kuwapa vifaa vya kisasa kutasaidiya pia serikali kuokoa mapato ya kodi yaliokuwa yakipotea kupitia bidha zinazoingizwa nchin kimagendo. Hakusahau kutilia maanani suala la usalama katika aneo lenye visima vya mafuta la Ziwa Albert, karibu na pori za DRC, zilizonyumbani kwa wasi wa Uganda wa ADF wenye uhusiano na magaidi wa kimataifa.

Maafisa hamsini ndiyo wametangulia kupata mafunzo ya mwezi mmoja katika chuo hicho. Uganda ambayo iliwahi kushambuliwa na magaidi, imeimarisha zaidi usalama wake kufuatia shambulio la Westgate jijini Nairobi-Kenya na wanamgambo wa Kisomali wa Al-shabab.