Tunaweza kushughulikia tofauti zetu na Marekani: Rais Rouhani

24 Septemba 2013

Suala la uhusiano waIran na Marekani pamoja na mpango wa nyuklia wa nchi hiyo ni miongoni mwa mambo yaliyokuwemo kwenye hotuba ya Rais Hassan Rouhani wa Iran alipohutubia kwa mara ya kwanza mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, tangu achaguliwe kushika wadhifa huo hivi karibuni.

Rais Rouhani amesema fikra za kwamba mpango wa nyuklia waIranni wa matumizi mengineyo kando ya matumizi salama ni potofu na kamwe hawajawahi kufanya hivyo. AmesemaIraninasisitiza haki yake ya kuendeleza mradi wake na iko tayari kushiriki mara moja kwa muda utakaopangwa katika mazungumzo ya kujenga kuaminiana, ya usawa na ya uwazi.

AmesemaIraninasaka ubia na nchi zenye maslahi sawa na haina lengo la kuongeza mvutano na Marekani huku akisema kuwa amemsikiliza kwa makini Rais Barack Obama katika hotuba yake kwa baraza kuu na hivyo..

(Sauti ya Rouhani)

 “Tunaweza kufikia muundo wa kushughulikia maliza tofauti zetu. Kwa mantiki hiyo, mazingira sawia, kuheshimiana na kutambua sheria za kimataifa vinapaswa kuongoza mashauriano hayo. Na bila shaka tunatarajia kupata msimamo usiobadilikabadilika kutoka Marekani."