Shambulio la kigaidi Westgate Kenya ni changamoto ya Kimataifa:

24 Septemba 2013

Shambulio la kigaidi lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kenya limepewa uzito wa juu kwenye mkutano wa viongozi wanaojadili malengo ya maendeleo ya milenia kwenye Baraza Kuu la Umoja wa mataifa. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Kwa pamoja viongozi hao wamelaani vikali unyama uliokatili maisha zaidi ya 60 na kujeruhi wengine zaidi ya 150. Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernad Membe ni miongoni mwa viongozi waliojadili suala hilo

(SAUTI YA BERNAD MEMBE)

Mbali ya suala la Kenya kikao cha 68 cha mjadala wa marais kinajikita katika uchambuzi wa ajenda kuu nne kwa mujibu wa Membe

(SAUTI YA MEMBE CLIP 2)