Malawi yapiga hatua katika kuwajumuisha walemavu kwenye ajenda ya maendeleo

24 Septemba 2013

Tatizo la ulemavu ni kubwa , ikikadiriwa kuwa watu takribani   watu bilioni moja wanaishi na aina Fulani ya ulemavu. Kila nchi   inachagizwa na Umoja wa Mataifa kuhakikisha mipangoyaoya baada ya mwaka 2015 inajumuisha mahitaji na mchango wa walemavu katika kuleta maendeleo endelevu, kwani bila kuwakwamua walemavu maendeleo endelevu itakuwa ni ndoto.

Mataifa mbalimbali sasa yameanza kuchukua hatua za kuhakikisha ajenda hiyo inapewa kipaumbele na Malawi ni miongoni mwa nchi hizo kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa viongozi kuhusu ulemavu hapa kwenye Umoja wa mataifa imewakilishwa na viongozi wa serikali, watu wenye ulemavu na jumuiya mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali kama sight savers na Virginia ni mwakilishi wake

 (SAUTI YAVIRGINIA)

“NchiniMalawi kuna mikakati mingi inayoendelea kuhakikisha watu wenye ulemavu wanajumuishwa katika sera za maendeleo za taifa , mfano hivi karibuni sheria ya masuala ya ulemavu imepitishwa  ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanajumuishwa kwenye mikakati ya maendeleo na Sight savers wameshiriki kwa kiasi kikubwa kugfanya kazi na wajumbe wengine."