Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 690 wauawa katika machafuko ya Boko Haram Nigeria tangu Mai:OCHA

Watu 690 wauawa katika machafuko ya Boko Haram Nigeria tangu Mai:OCHA

Machafuko na ukosefu wa utulivu unaendelea Kaskazini Mashariki mwaNigeriakukiwa na mapigano zaidi baina ya kundi la kidini la Boko Haram na vikosi vya serikali na washirika wake. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa Agost na shirika la Umoja wa mataifa la masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura OCHA idadi ya imeongezeka kwa watu 153 waliouawa katika mashambulio saba na kufanya jumla ya watu 690 kupoteza maisha yao tangu kutangazwa kwa hali ya dharura huko Yobe, Borno, na Adamawa Mai mwa ka huu. George Njogopa na taarifa zaidi

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Mamia ya watu wamelazimika kukimbilia majimbo ya mbali kuomba hifadhi huku wengine wakivuka mipaka  na kuingia nchi za Chad, Cameroon na Nigeria, kutokana na machafiuko hayo ambayo baadhi yametokea katika majimbo ya Yobe, Borno na Adamawa ambayo mwezi wa May mwaka huu yalitangazwa kuwa katika hali ya hatari.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema kuwa, kunzia kipindi cha mwezi May hadi sasa limewapata watu 17,000 wasio kuwa na makazi wengi wao wakiwa wanawake na watoto .

Juhudi za mashirika kutoa misaada ya kiutu kusambaza misaada ya dharura katika eneo la kkaskazini zimeshindwa kufua dafu kutokana na kukosekana kwa hali ya usalama.

Hata hivyo, OCHA, ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya misaada ya usamaria wema, limesema kuwa limepata taarifa kuwa baadhi ya mashirika hayo ya misaada yamechukua mbinu ya ziada kwa kuanzisha mashirikiano na taasisi za eneo hilo kwa ajili ya kufanikisha mipango ya usambazaji huduma za kibinadamu.