Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya Pinheiro inachunguza matumizi ya silaha za kemikali Syria

Tume ya Pinheiro inachunguza matumizi ya silaha za kemikali Syria

Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limejulishwa hii leo kwamba Tume ya kimataifa ya uchunguzi dhidi ya Syria inafanya uchunguzi wake huru kubaini nani anahusika na shambulio la kemikali la tarehe 21 Agosti 2013 kwenye viunga vya mji mkuu Damascus. Mwenyekiti wa Tume hiyo Sérgio Pinheiro ameeleza hayo pamoja na kile ambacho wamebaini kuhusu madhila yanayokumba wananchi wa Syria. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Jason)

Akihutubia baraza la haki za binadamu mjini Geneva mwenyekiti wa tume hiyo Sergio Pinheiro amesema kuwa matumizi ya silaha za kemikali ni uhalifu wa kivita. Amesema kuwa wananchi wa Syria wanakabiliwa na mashambulizi ya mabomu kutoka kwa vikosi vya serikali huku wanamgambo wakiyalenga raia maeneo ya kaskazini. Miji mingi imebaki kuzingirwa huku mateso yakiendeshwa kwenye vizuizi vya serikali.

Bwana Pinheiro anasema kuwa vikosi vya serikali wakiwemo wanamgambo hawaheeshimu sheria zinazostahili kufuatwa wakati wa vita zinazozuia kushambuliwa kwa maeneo walioko raia kama vile hospitali.

 (SAUTI YA PINHEIRO)