Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto Milioni 90 wamepuka vifo duniani, Tanzania imo: UNICEF

Watoto Milioni 90 wamepuka vifo duniani, Tanzania imo: UNICEF

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limetoa ripoti mpya inayoonyesha kuwa watoto Milioni 90 walio na umri wa chini ya miaka mitano wameepuka vifo kutokana na hatua zilizochukuliwa na serikali na mashirika mbali mbali. Ripoti ya Alice Kariuki inaeleza zaidi.

(Ripoti ya Alice)

Ripoti hiyo inasema kuwa idadi ya vifo vya watoto hao kwa mwaka imepungua kutoka Milioni 12 nukta Sita mwaka 1990 hadi Milioni Sita nukta Sita mwaka jana.  Mkurugenzi Mkuu wa Unicef Antony Lake anasema kupungua kwa idadi hiyo kunatokana na upatikanaji wa tiba, chanjo na kuimarishwa kwa lishe na elimu kwa wakina mama hususan wajawazito. Amesema taarifa hizo ni za kufurahia na kitendo cha kufikisha huduma bora za mtoto kwa watu wasio na uwezo kimesaidia zaidi. Geeta Rao Gupta ni Naibu Mkurugenzi wa UNICEF

 (Sauti  ya Rao)

 Tanzania ni moja ya nchi zilizotajwa kupata mafanikio ya kupunguza vifo vya watoto wachanga na Sudha Sharma Mkuu wa masuala kwa UNICEF Tanzania ina mipango mizuri ya Malaria dhidi ya watoto pamoja na chanjo akitaja uhifadhi ni mojawapo ya siri za mafanikio.

 (Sauti ya Sudha)

 “Tanzania imechukua hatua kadhaa kuhakikisha chanjo zenye ubora zinahifadhi  ubora wake, kuna majokofu yanayotumia nishati ya jua, gesi na UNICEF kwa ushirika na wadau wake imesaidia kuimarisha huduma,  katika kila mkoa wa Tanzania kuna vyumba vya baridi kwa ajilia ya kuhifadhi chanjo.