Misaada ya kibinadamu yafikishwa Myanmar kwa mara ya kwanza : OCHA

10 Septemba 2013

Ofisi ya Umoja wa kimataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema magari kumi na moja yaliyoko chini ya UM na washirika wengine wa maswala ya kibiadamu yamesambaza chakula , madawa na vitu vingine kwa jamii zilizopoteza makazi huko Mynamar.Taarifa zaidi na George Njogopa

(TAARIFA YA GEORGE)

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya eneo hilo kuruhusiwa kupita kwa msafara huo ambao wamefanikiwa kusambaza huduma za dharura katika eneo la Laiza, tangu mwaka 2011.

Machafuko katika jimbo la Kachin na eneo la Kaskazini mwa jimbo la Shan yamesababisha kiasi cha watu 100,000 kukosa makazi.

Hadi sasa idadi ya watu waliosajiliwa kwenye makambi inafikia 91,000 ikiwemo pia wale 53,000 ambao hawafikiwa na msaada wa serikali

Tangu kuanza kwa machafuko hayo mwaka 2011 kumekuwa na ujumbe unaotembelea mara kwa mara katika maeneo ya mipakani ambao hata hivyo ujumbe huo haukufanikiwa kuzuru maeneo mengi zaidi. Yens Laerke ni msemaji wa OCHA

(SAUTI YA YENS LAERKE)