Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Meja Jenerali Edy Mulyono mkuu wa kikosi cha MINURSO

Ban amteua Meja Jenerali Edy Mulyono mkuu wa kikosi cha MINURSO

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu inasema Meja Jenerali Mulyono anachukua nafasi ya Meja Jeneral Abdul Hafiz wa Bangladesh, ambaye amekamilisha majukumu yake July 23 mwaka huu. Bwana Ban amemshukuru kwa utumishi na mchango wake ndani ya MINURSO.

Mteule huyo mpya ana uzoefu wa kitaifa na kimataifa katika masuala ya kijeshi akiwa ameshika nafasi mbalimbali za kijeshi.