Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM ataka Belarus imwachilie Ales Bialiatski

Mtaalamu wa UM ataka Belarus imwachilie Ales Bialiatski

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Belarus, Miklós Haraszti, ameitaka serikali ya jamhuri hiyo kumuachilia mara moja na bila masharti mpigania haki za binadamu Ales Bialiatski.

Kwa mujibu wa mwakilishi huyo kushikiliwa kwa bwana Bialiatski ni ishara ya ukandamizaji wa watetezi wa haki za binadamu. Miaka miwili iliyopita mnamo Agost 4 mwaka 2011 bwana Bialiatski,mkuu wa kituo cha haki za binadamu cha Viasna, aliswekwa rumande mjini Minsk kwa makosa ya ukwepaji kodi.

Na baadaye mwaka huo akahukumiwa kwenda jela miaka mine na nusu na kupokonywa kila kitu zikiwemo rasilimali zilizoandikishwa kwa watu wengine. Hukumu hiyo ilizingatiwa kati rufaa iliyokatwa mwaka 2012.

Mtaalamu huyo amesema kukifilisi kituo cha Viasna ni ukiukwaji wa uhuru wa kujumuika ambao umewekwa bayana katika mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na kisiasa.